Baraza la Mpira wa Miguu kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (Cosafa), limetoa zawadi ya dola 10,000 kwa Taifa Stars ya Tanzania baada ya kushinda na kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya Castle Cosafa yaliyofanyika mwezi uliopita nchini Afrika Kusini.

Fedha hizo ni sawa na Sh. mil 22,000,000 za kitanzania, ambapo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeamua fedha hizo kwa mgawanyo sawa, zitolewe kwa wachezaji wote walioshiriki fainali hizo pamoja na benchi la ufundi.

Aidha, Cosafa imetuma fedha za zawadi kwa wachezaji wa Tanzania ambao walifanya vizuri kwenye mchezo mmoja baada ya mwingine katika mashindano hayo ambayo yalikuwa na mvuto wa aina yake kwa mafanikio ya timu ya Tanzania.

Wachezaji hao ni Shiza Kichuya aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Malawi, Muzamiru Yassin aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Angola, Erasto Nyoni aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Mauritius na Elius Maguri aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Afrika Kusini.

Hata hivyo, Kipa Bora wa michuano hiyo ni Said Mohammed aliyezawadiwa moja kwa moja na Cosafa, ambapo Tanzania ilishika nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa Zimbabwe na Zambia iliyoshika nafasi ya pili.

Jumba la professa J lapitiwa na bomoaboma, lapigwa X
Hatma ya Kagame kujulikana leo, raia wapiga kura