Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kimeanza safari ya kuelekea Binin, tayari kwa mchezo wa mzunguuko wa nne wa ‘Kundi J’ wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022.

Wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi wameondoka jijini Dar es salaam leo mchana kwa usafiri maalum wa Ndege ya Shirika na Ndege la Tanzania ‘Air Tanzania’ aina ya Airbus A220-300.

Stars inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen ina kibarua cha kwenda kusaka pointi tatu mbele ya Benin kwa ajili ya kuwania tiketi ya kucheza Kombe la Dunia Qatar 2022.

Katika mchezo uliochezwa jana Alkhamis (Oktoba 7), Stars ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0, hivyo ina kibarua kizito cha kusaka ushindi ugenini.
Poulsen amesema kuwa anawaamini vijana wake wanaweza kupata matokeo kwenye mchezo huo kwa kuwa makosa ambayo wameyafanya watayafanyia kazi.

“Makosa ambayo tumeyafanya kwenye mchezo wa mwanzo tutayafanyia kazi ili kuweza kupata ushindi kwenye mchezo wetu wa marudio.

“Vijana walikuwa wanahitaji ushindi ila walikwama kumalizia nafasi ambazo walitengeneza hivyo bado tuna muda wa kufanya kwenye mechi ijayo,” amesema Kim Poulsen.

Baada ya michezo ya Jana Alkhamis (Oktoba 07), Msiammo wa Kundi J unaonesha Benin inaongoza ikiwa na alama alama 7, ikifuatiwa na DR Congo yenye alama 5 huku Tanzania ikiwa nafasi ya tatu na alama zake 4 na Madagascar inaburuza mkia, baada ya kupoteza michezo yote mitatu.

Vitanda vya umeme vyapokelewa kusaidia wagonjwa kansa Ocean Road
Wangeona mafunzo mlionayo wasingethubutu - IGP Sirro