Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo kimepoteza alama tatu baada ya kufungwa na Lesotho 1-0, katika mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki Kombe la Mataifa Huru barani Afrika nchini Cameroon.

Taifa Stars ambayo ilikuwa ugenini, ilionesha kiwango kilichowapa matumaini Watanzania hasa katika kipindi cha kwanza, lakini makosa yaliyofanywa katika dakika ya 76, yaliwapa Lesotho goli lililotokana na mpira wa kona.

Matokeo hayo yanaiweka Tanzania katika nafasi ya nne kwenye kundi ikiwa na alama 5 sawa na Lesotho, na alama 1 mbele ya Cape Verde.

Tanzania bado inayo nafasi ingawa ni finyu zaidi kwa sasa kutokana na matokeo ya leo. Inajipanga kucheza na vinara wa kundi hilo, Uganda Cranes.

Uganda tayari wameshajipatia nafasi ya kuingia Cameroon, inaongoza kundi ikiwa na alama 13 ambazo ni zaidi ya mara mbili ya Tanzania au Lesotho.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe alihudhuria mtanange huo kuwatia moyo Taifa Stars.

Watu maarufu wametumia mitandao ya kijamii kuwatia moyo Taifa Stars kutokana na matokeo hayo, wakiwataka wajipange tena kwani nafasi bado ipo.

Video: Hamisa aachia 'Tunaendana' akiwa na mpenzi wake, ni kiki au penzi?
Waziri Mwakyembe aitaka Taifa Stars kutowaangusha Watanzania