Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Kim Poulsen ametaja kikosi cha timu hiyo, kwa ajili ya mchezo wa mzunguuko wa tatu wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Benin.

Stars itacheza mchezo huo wa kundi J Oktoba 07 huku ikiwa na kumbukumbu ya kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya DR Congo kisha kuichapa Madagascar mabao 3-2.

Mhezo huo kwa Stars utachezwa ugenini mjini Cotonou katika uwanja wa taifa (Stade de l’Amitié).

Mpaka sasa Tanzania inaongoza msimamo wa kundi J ikiwa na alama 4 sawa na Benin inayoshika nafasi ya pili, lakini timu hizo zimetofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

Nafasi ya tatu inashikwa na DR Congo yenye alama 2 huku Madabascar ikiburuza mkia baada ya kupoteza michezo yake dhidi ya Benin na Tanzania.

Chris Mugalu awajibu wanaombeza
Ramsey kuingizwa sokoni Januari 2022