Timu ya Taifa ya DR Congo imeiduwaza Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kwa kuichapa nyumbani mabao 3-0, katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022.

Taifa Stars iliyokua inaongoza msimamo wa Kundi J kabla ya mchezo huo, imeruhusu mabao hayo katika dakika ya 6, 66 na 85.

Mabao ya DR Congo iliyokua ugenini Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam yamefungwa na Gael Kakuta, Nathan Idumba Fasika, Ben Malango.

Kupoteza mchezo huo kwa mabao 3-0 kumeifanya Taifa Stars ipoteze matumaini ya kumaliza kinara wa Kundi J, kwani hivi sasa kundi hilo linaongozwa na DR Congo iliyofikisha alama 8, huku Benin yenye alama 7 ikitarajia kucheza baadae dhidi ya Madagascar.

Taifa Stars itacheza mchezo wa mwisho dhidi ya Madagascar mjini Antananarivo Jumapili (Novemba 14), huku DR Congo ikitarajiwa kucheza nyumbani dhidi ya Benin siku hiyo hiyo.

Mbowe na wenzake washinda pingamizi
Fursa za ajira Tanga