Akaunti ya pesa ya Tailor Swift imenona mwaka huu kuliko ya mtu yeyote maarufu na kumfanikisha kushika nafasi ya kwanza kwenye orodha ya Forbes yenye watu 100 maarufu duniani waliotengeneza pesa ndefu zaidi (100 highest-paid celebrities 2016).

Kwa mujibu wa Forbes, Tailor Swift ametengeneza $170 milioni tangu Juni 2015, kutokana na kazi zake za sanaa akipiga matamasha makubwa katika majiji mbalimbali duniani. Ziara yake aliyoibatiza ‘1989 Tour’ ndiyo iliyomuinua zaidi.

Tailor amewapita kwa mbali kundi la One Direction lililotengeneza kiasi cha $100 milioni na kuwa kundi la muziki lililoingiza pesa ndefu zaidi duniani, huku nafasi tatu ikienda kwa mwandishi maarufu wa vitabu, James Patterson akiwa ameingiza kiasi cha $95 milioni. Mwandishi huyo pia ametajwa kuwa mtu maarufu ambaye yuko ‘bize’ zaidi.

Soka halikuachwa nyuma kwenye orodha hii, limeongozwa na Mreno Cristiano Ronaldo (Cr7) ambaye amefanikiwa kutengeneza kiasi cha $88 milioni. Ronaldo ameshika nafasi ya 5 afuatana na Dk. Phil McGraw aliyetengeneza $88 milioni pia. Mpinzani wake katika soka, Lionel Messi ameshika nafasi ya 8 akiwa ameingiza kiasi cha $81.5.

Ronaldo

Tasnia ya vichekesho imewakilishwa vyema na Kevin Hart,aliyeshika nafasi ya 6 akiingiza kiasi cha $87.5 milioni. Amekuwa mchekeshaji wa kwanza kufikia rekodi hiyo ya pesa akipiga matamasha makubwa katika ziara ambazo hazijawahi kuingiza pesa nyingi kwa ucheshi.

Muigizaji mkongwe na mfalme wa filamu nchini China, Jackie Chan ameibuka kwenye orodha hii licha ya kutotoa filamu nyingi mpya kama zamani. Ameshika nafasi ya 23 akiingiza $61 milioni. Jackie Chan anatajwa kuwa muigizaji wa pili aghali zaidi duniani. Kazi ya uongozaji wa filamu za mapigano pamoja na biashara zake vimetajwa kama chanzo.

Jackie CHAin 2

Waimbaji wengine waliong’ara kwenye orodha hiyo ni Adele aliyeshika nafasi ya 9 ($80.5 milioni), Madonna akishika nafasi ya 12 ($76.5 milioni). Rihanna amemfuatia Madonna katika nafasi ya 13 ($75 milioni) na Katy Perry aliyeshika nafasi ya 63 ($41 milioni).

Beyonce amejikuta katika nafasi ya 34 akiwa ameingiza $54 milioni, zaidi ya mumewe Jay Z ambaye ameshika nafasi ya 36 akiwa ameingiza $53.5.

Beyonce

 

 

Kikosi Bora Cha Euro 2016 Chatajwa
Aldo Agroppi: Nashangaa Kuona Klabu Inajipangia Ada Ya usajili