Hivi karibuni Tailor Swift alijikuta akikabiliwa na tuhuma za wizi wa mashairi ya wimbo wake ‘Shake It Off’ kutoka kwa msanii aitwaye Jesse Braham, aliyedai kuwa Tailor alidokoa kutoka kwenye wimbo wake ‘Haters Gone Hate’ wa mwaka 2013.

Braham alidai kuwa Tailor Swift alichukua shehemu ya maneno katika mashairi yake na kuyarudia zaidi ya mara 70 kwenye wimbo wake, hivyo alidai kurejeshewa fidia ya $42 million.

Sehemu anayodai msanii huyo ni maneno yaliyoko kwenye kibwagizo,”Haters gone hater, playas gone play. Watch out for them fakers, they’ll fake you everyday.”


Hata hivyo, Taarifa zilizotolea jana na chanzo cha kisheria kimeleza kuwa Bw. Braham hana haki ya kudai mashairi hayo. Kimeeleza kuwa kwa sheria ya hati miliki haizuii matumizi ya maneno mafupi na kwamba maneno hayo yaliyochukuliwa na Tailor Swift sio maneno yaliyoanzishwa na mlalamikaji.

Hivyo, nyimbo hizo mbili zinaonekana kutokuwa na uhusiano wa aina yoyote.

Rapper Wa Marekani Aliyejiunga Na ISIS Auwawa, Ni Rafiki Wa DMX
Wizkid: R. Kelly Aliomba Kunishirikisha Kwenye Wimbo Wake