Siku kadhaa baada ya kuibuliwa kashfa ya kupotea kwa makontena 349 bandarini yakiwa yamepitishwa kwenye bandari ya nchi kavu ya kampuni ya Said Bakhresa, tajiri mmoja amejitokeza na kukiri kumiliki baadhi ya makontena hayo.

Tajiri huyo anayetambulika kwa jina la Nassoro Ahmed bin Slum anayemiliki kampuni ya Bin-slum Tyres Ltd, amesema kuwa ni kweli anamiliki baadhi ya makontena yaliyokubwa na kashfa hiyo lakini kosa lenye sura ya kukwepa kodi limefanywa na wakala wake.

“Wafanyabiashara hatuna mamlaka ya kulipa kodi moja kwa moja serikalini. Tunalipa kodi kupitia kwa wakala aliyechaguliwa na serikali. Mimi nilimlipa kazi wakala wangu ambaye nimekuwa nikifanya naye kazi kwa miaka 10,” Bin Slum aliliambia gazeti la Raia Mwema.

“Mara kwa mara huwa ananiletea nyaraka za malipo ya kodi lakini kwenye mzigo huu wa sasa  ambao kontena zangu zina matatizo ya kodi, alinitangulizia mzigo na mimi nikamdai nyaraka. Yeye aliniambia ananiandalia faili,” alieleza.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliagiza wote wanaohusika na kashfa hiyo kukamatwa na kuchukuliwa hatua na kodi iliyokwepwa ilipwe.

Tayari watu 12 wanashikiliwa na jeshi la polisi kufuatia sakata hilo.

 

Profesa Jay Afunguliwa Kesi Mahakama Kuu
Dk Slaa Amzungumzia Rais Magufuli, Amshauri