Klabu ya African Lyon ya Dar es Salaam imepata Mwenyekiti mpya Mtendaji, ambaye mfanyabiashara mwenye wa Asia, Dk Sulaiman Al-Fahim.

Mmiliki wa African Lyon iliyopanda tena Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Rahim Kangezi amesema kwamba Dk. Al- Fahim amekubali ombi la kuwa kiongozi mkuu wa klabu hiyo ya zamani ya mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta baada ya kuombwa kwa miaka minne sasa.

Kangezi amesema waliamua kumuomba Al Fahim kuwa kiongozi mkuu wa klabu yao si kwa sababu mfanyabiashara mkubwa na bilionea nchi za Uarabuni na duniani kwa ujumla, bali pia kutokana na uzoefu wake katika michezo, hususan soka.

Amesema Al- Fahim ni Rais wa kampuni ya Arab Union for Real Estate Development ya Dubai baada ya awali kuwa Msemaji wa kampuni Abu Dhabi United Group (ADUG), wamiliki Manchester City ya England walioinunua Septemba, 2008.

Kangezi amesema Al- Fahim aliyejaribu bila mafanikio kununua Portsmouth iliyowahi kushiriki Ligi Kuu England, ataanza kazi rasmi African Lyon Aprili 16 kwa kutangaza timu atakayofanya nayo kazi.

Dk Shein kufungua leo baraza la wawakilishi akiwa na kitendawili
Wanaosakwa kwa wizi wa mabilioni Uingereza waishi Tanzania kwa utulivu