Mabingwa wa soka nchini Ufaransa, Paris Saint-Germain hawajakata tamaa ya kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo.

PSG wametajwa kuendelea na mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo hatari kwa kuamini ana nafasi kubwa ya kuwa sehemu ya kikosi chao msimu ujao wa ligi, baada ya kuondoka kwa Zlatan Ibrahimovic.

Tayari kiasi cha Euro milioni 120 kimetengwa na matajiri hao wa jijini Paris kwa ajili ya kuhakikisha wanaipata saini ya Ronaldo.

Msukumo mkubwa wa mipango ya usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, umekuwa ukitolewa na mmiliki wa PSG, Nasser Al-Khelaïfi ambaye aliwahi kukiri kuvutiwa na Ronaldo.

Hata hivyo huenda PSG wakakutana na kizuizi kutoka kwa Real Madrid, kutokana na klabu hiyo kutoonyesha dalili zozote za kumuweka sokoni Ronaldo katika kipindi hiki cha kuelekea majira ya kiangazi.

Ronaldo alisajiliwa kwa Real Madrid mwaka 2009 akitokea Man Utd kwa ada ya uhamisho wa Pauni milioni 80 ambayo kwa wakati huo ilimpa sifa ya kuwa mchezaji aliyesajiliwa kwa kiasi kikubwa cha pesa.

Audio: Jay – Z airukia ‘All the Way Up’ ya Fat Joe na Remy Ma
Usajili Wa Zlatan Ibrahimovic, Man Utd Kutumia Kivuli Cha Mourinho