Viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamekutana na wadau mbalimbali wa kudhibiti taka ngumu kwa lengo la kujadili namna ambayo wanaweza kukusanya taka na kuzifanya kuwa shughuli ya biashara na ajira.

Hayo yamesemwa jijini Dar e4s salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba ambapo amesema kuwa mfumo wa ukusanyaji taka ni muhimu hasa serikali kuweka mazingira ya kisera, kisheria na kiuchumi ili takataka ziwe mali.

“Tumeona watu wanaokusanya taka mtaani na katika majumba yetu kila siku muda mwingine tunawaona kama vichaa kutokana na kuokota taka hizo ikiwemo makopo lakini hiyo ni shughuli ya ajira na ya kipato na tunaamini kwamba ilasimishwe”. Amesema Makamba.

Aidha, amesema kuwa miundombinu ya miji lazima iboreshwe hasa wao kama serikali wanajukumu la kuboresha miundombinu ikiwemo madampo, mifereji pamoja na kuweka sehemu ya kutupa na kukusanya.

“Sera, sheria, kanuni na taasisi kwamba suala la ukusanyaji wa taka na udhibiti wa taka lazima lifanywe na taasisi mahususi kwa ujumla na lazima kuwepo na sheria ikiwemo sheria ndogo na sera ambazo zitawezesha shughuli ya taka iwe biashara na ifanyike kwa urahisi.

Kwa upande wa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Utafiti, Profesa Cathbert Kimambo amesema kuwa mkutano huo ambao umewashirikisha wadau wa nje na ndani watajadili na kusambaza taarifa na matokeo ya kitafiti na yakitaalamu kuhusu masuala ya ukusanyaji wa taka ngumu.

Vilevile upande wa Mratibu wa kitengo cha tafiti za sera na utetezi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam shule kuu ya biashara Dkt. Goodluck Charles amesema katika tafiti ambazo zimefanyika ni kuangalia njia za kuboresha masuala ya kukusanya, kusafirisha na kuchakata taka ngumu katika jiji la Dar es Salaam na katika majiji mengine.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Aprili 30, 2019
Video: Zingatia haya kabla haujanunua Masofa nyumbani kwako

Comments

comments