Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Pwani, imemfikisha mahakamani, Romani Michael Jovin ambaye ni (volunteer surveyor ) wa DAWASA kwa kosa la kuomba rushwa ya sh. 70,000 na kupokea rushwa ya kiasi cha sh. 50,000.
 
Mtumishi huyo amejikuta akifikishwa kizimbani baada ya kwenda kinyume na kifungu cha 15(1) (a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba. 11 ya mwaka 2007.
 
Aidha, Romani Michael ambaye alifunguliwa kesi ya jinai mamba 140 ya mwaka 2018 ni volunteer Surveyor DAWASA Ubungo.
 
Akisoma mashtaka hayo mbele ya hakimu mkazi wilaya ya Kibaha, Herieth Mwailolo, mwendesha mashtaka wa TAKUKURU, Prisca Mpeka ameileza mahakama kwamba mshitakiwa alitenda kosa la kuomba rushwa ya sh.70,000 na kupokea rushwa ya sh. 50,000 kutoka kwa mtoa taarifa ili aweze kumsaidia mtoa taarifa kupata mita ya DAWASA.
 
Amesema kuwa jambo hilo ni kosa kisheria kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa, sheria namba 11 ya mwaka 2007.
 
  • Serikali yazindua Viza na vibali vya ukaazi vya kielektroniki
 
  • Nyuki wamshambulia kikongwe hadi kufa
 
  • Mikoa ambayo magereza yake yatalima Mahindi, Maharage na Mpunga yatajwa
 
Hata hivyo, Mshitakiwa amekana makosa yote mawili na dhamana iko wazi, na mshtakiwa huyo ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana na hivyo amepelekwa gerezani mpaka atakapotimiza masharti ya dhamana.

Video: Tumekusudia kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya Kilimo- Hasunga
Gattuso aendelea kumkana Zlatan Ibrahimovic