Hekaheka za kura za maoni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) zimeendelea kugubikwa na matukio mbalimbali katika hatua za kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali ambapo tuhuma za rushwa zimekuwa sehemu ya mchakato huo.

Naibu waziri wa fedha na mbunge wa Iramba Magharibi ameshikiliwa na kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Singida kwa tuhuma za kukiuka Sheria ya Gharama za  Uchaguzi na sheria ya Kupambana na Rushwa namba 1 ya mwaka 2007.

Mkuu wa Takukuru mkoa wa Singida, Joshua Msuya alithibitisha kuwa taasisi hiyo inamhoji Mwigulu Nchemba kuanzia juzi kufuatia tuhuma hizo.

Msuya alisema kuwa taasisi hiyo ilichukua hatua hiyo kutokana na malalamiko yaliyowasilishwa na David Jairo, Amon Gyuda na Juma Kilimba ambao ni wapinzani wake. Wagombea hao waliieleza Takukuru kuwa Mwigulu Nchema alikuwa akitoa ahadi mbalimbali na kuwapa wananchi Pikipiki na baiskeli kama sehemu ya zawadi za kuwashawishi.

Ilielezwa kuwa Nchimbi aliwanunua wasimamizi wa uchaguzi wa eneo hilo ambao walionekana kumpendelea katika mambo mbalimbali huku wakiwapuuza wagombea wengine. Uongozi wa CCM ulichukua uamuzi wa kuwaondoa wasimamizi hao baada ya kuibuka tuhuma hizo ili kuhakikisha uchaguzi huo unafuata sheria na kuweka usawa kwa wote.

Mbowe Na Lowassa ‘Waliudanganya’ Umma Kuivuruga CCM
Perez Na Ramos Wamalizana, Sasa Mambo Shwari