Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeanza kuchunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Brig. Jen. John Mbungo amesema wameanza uchunguzi huo kutokana na taarifa walizonazo kama kuna matumizi mabaya ya fedha za michango ya wanachama, wanayochanga kwa mujibu wa Katiba yao.

Amebainisha watakaohojiwa ni dkt. Vincent Mashinji, aliyekuwa katibu mkuu CHADEMA, kwa sasa amehamia CCM, John Mrema, mkurugenzi wa itifaki na mambo ya nje na dkt. Roderick Lutembeka, mhasibu wa chama hicho.

Aidha, Mkurugenzi huyo amesema wameshindwa kumhoji mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwa kuwa aliieleza TAKUKURU kwamba yuko nje ya jiji la Dar es salaam.

Amesema, Taasisi hiyo imeshaanza kukusanya nyaraka kutoka sehemu mbalimbali huku akisema imekuwa ikipata ushirikiano mzuri kwenye suala hili.

Hata hivyo, naibu katibu mkuu wa CHADEMA Bara, Benson Kigaila, amekanusha tuhuma hizo akisema hakuna uthibitisho unaoonesha chama hicho kina matumizi mabaya ya fedha.

Boti za Zanzibar I, II zasitisha safari baada ya kupata hasara
Lipuli FC kuanzia Iringa