Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) inajiandaa kuanza kutoa elimu ya madhara ya rushwa kuanzia ngazi ya shule ili kuandaa Taifa la baadaye.

Hayo yamesemwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola wakati wa uzinduzi wa utoaji wa huduma kwa umma Mkoani Dodoma, ambapo amesema taifa lolote duniani lenye rushwa huwa halina amani kwa sababu ya wananchi kutofuata utaratibu na sheria za nchi.

“Ili kuwa na taifa la baadaye lisilo na rushwa, TAKUKURU tunajikita kuwekeza nguvu kwa watoto kwa kutoa elimu ya kupambana na rushwa ili kuongeza kasi kubwa ya maendeleo ya nchi na jamii ishiriki katika elimu hii,”amesema Mlowola

Aidha, Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Dodoma, Emmanuel Kuboja akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge, amesema  serikali ya Tanzania imedhamiria kuidhiirishia dunia kwamba, itasimamima kwa vitendo dhana na misingi ya uadilifu, haki za ubinadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa.

Hata hivyo, kwa upande wa Jeshi la Polisi Kamishina Msaidizi wa Polisi, Philip Kalangi amesema dhamira ya Jeshi la hilo ni kuhakikisha vitendo vya rushwa vinatokomezwa kwenye jamii na raia wote kuishi kwa haki na usawa.

Dodoma kuwa mwenyeji sherehe za uhuru
Magazeti ya Tanzania leo Desemba 7, 2017