Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Lindi imepokea jumla ya taarifa za malalamiko yanayohusu vitendo vya rushwa 47 huku majalada manne uchunguzi wake ukikamilika katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2018/2019.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa TAKUKURU mkoani Lindi, Stephen Chami wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kuanzia January hadi Marchi 2019.

Amesema kuwa kuanzia January hadi marchi mwaka huu TAKUKURU imefanikiwa kufungua jumla ya kesi mpya (3) zikihusisha sekta ya afya na serikali za mitaa huku kesi 14 zikiendelea mahakamani na ziko katika hatua mbalimbali za utekelezaji kisheria.

Aidha, sambamba na hilo katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2018/2019 TAKUKURU mkoa wa Lindi inafuatilia miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 8, 180, 718, 289/=  ikihusisha ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Lindi eneo la Kiwalala na daraja la Lukuledi Wilayani Ruangwa.

Hata hivyo, ameongeza kuwa TAKUKURU mkoa wa Lindi inaendelea kufuatilia mradi Wa ujenzi Wa ujenzi Wa Hospital ya wilaya ya Lindi inayojengwa katika eneo la Kiwalala ambayo itagharimu shilingi billioni moja na millioni mia tano na mradi huo unasimamiwa na Halmashauri ya wilaya ya Lindi kwa kutumia Force Account.

Wananchi wajenga vyumba vitano vya madarasa wilayani Mtwara
Taasisi za Umma zaongoza kwa kudaiwa bili ya maji Tarime

Comments

comments