Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) Meja Generali John Mbung’o ametoa tahadhari kwa wagombea uongozi nafasi mbalimbali wanaotaka kuchaguliwa kwa kutoa rushwa.

Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Takukuru Makao Makuu jijini Dodoma leo Juni 17,2020.

Ambapo amesema kuwa Rais John Magufuli ni kiongozi ambaye anapambana na kuchukia rushwa na alijipambanua hata alipozindua Bunge la 11 mwaka 2015 na alishaonyesha msimamo kwa viongozi wake ambao angewateua kwamba asingekuwa na simile kwa kiongozi atakayejihusisha na rushwa.

“Ukimchagua mtoa rushwa akipata nafasi anafikiria kurudisha fedha zake alizotumia na siyo kuwatumikia wananchi kwa kuwaletea maendeleo” amesema Generali Mbung’o

“Mbunge au Diwani amefanya nini katika muda wa uongozi wake, kama hajafanya kitu hakuna sababu ya kumrudisha madarakani.”amesema Generali Mbung’o

Aidha amesisitiza kwamba rushwa yoyote inaweza kumgharimu mwananchi kwa kutokuwa mtatuzi wa changamoto zinazomkabili.

Marekani: Rais Trump asaini amri ya mageuzi Idara ya Polisi
Mama Samia kuhudhuria kuapishwa Rais wa Burundi kesho