Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Njombe inawashikilia watumishi watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Francis Namaumbo kwa tuhuma za upotevu wa zaidi ya milioni 569 pamoja na makosa mengine ya uhujumu uchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Njombe, Charles Nakembetwa amesema kuwa watumishi hao wanashikiliwa kwa ajili ya uchunguzi.

‘’Wanachunguzwa kwa makosa chini ya vifungu 22, 23 na 28 vya kuzuia na kupambana na rushwa na. 11 ya mwaka 2007, ili kuimarisha na kudhibiti ukusanyaji wa mapato yake,”amesema kamanda Nakembetwa

Amesema kuwa TAKUKURU Mkoa wa Njombe imeweza kubaini katika halmashauri ya wilaya ya Makete shilingi milioni 569,537,072 sawa na 46% zilizokusanywa kwa utaratibu wa POS kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2018 hazijulikani zilipo.

Aidha, Nakembetwa amesema kuwa taarifa za kibenki na za kimfumo wa kompyuta zianaonyesha kuwa fedha zilizoingizwa benki katika kipindi hicho kilitolewa bila maelezo kutoka kwa wahusika kuonyesha fedha hizo zilipelekwa wapi na kwa madhumuni gani.

Hata hivyo, ameongeza kuwa TAKUKURU kama chombo cha uchunguzi na mashtaka kitachukua hatua kali kwa watakaobainika kuhujumu mapato ya serikali mara baada ya uchunguzi utakapo kamilika ikiwa ni pamoja na kufungua kesi mahakamani.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 15, 2018
Video: BMT yatuma salamu kwa wenyeviti wa riadha wa mikoa