Maonyesho ya “International Afrika Epo Festival” maarufu kama “UMOJA WA AFRIKA” International Festival, yanatarajiwa kuanza Alhamisi September 1 hadi 4, 2022 katika viwanja vya Fest Platz mjini Tuebingen nchini Ujerumani kwa kuwahusuisha watanzania na wasanii mbalimbali.

Miongoni mwa wasanii hao ni wachoraji na wa bunifu wa picha ‘Visual Arts”, akiwemo, Chilonga Hajji na Meddy, mwanamitindo rafiki wa mazingira Diana Magesa na Bi. Rabiah Al-Karitty wote kutoka Tanzania.

Wanamitindo hao, kwa pamoja wamewahi kushiri maonyesho mengi ya kimataifa yakiwemo New York Fashion week,Unesco Paris, Ufaransa na Toronto Fashion week, ya nchini Canada.

Aidha, katika maonesho hayo vikundi vya sanaa za maonyesho na bendi za muziki zitanogesha shughuli nzima siku ya tukio, ikiwemo bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya “The Ngoma Africa Band” maarufu kama FFU inayoongozwa na mwanamuziki kamanda Ras Makunja.

Mwanamuziki wa mtindo wa Reggae kutoka Tanzania Saidon na The Train Band yenye maskani yake nchini ujerumani anatarajia kushiriki tamasha hilo, sambamba na Ali Bayo Traditional Group ya nchini Senegal.

Serikali, PLF waitwa meza ya mazungumzo
Baada ya ligi kuu Parimatch yagawa upendo kwa wateja