Tamasha la Utamaduni la jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST, kwa mara ya kwanza linafanyika Nchini Tanzania mwezi wa tisa mwaka huu, kwa kukutanisha Nchi zote sita za jumuiya ya Afrika mashariki.

Katika tamasha hilo wasanii wote wanaojihusisha na shughuli za kiutamaduni watapata nafasi za kuonesha utamaduni na asili ya taifa lake, kwa vitu kama bidhaa, ngoma za utamaduni, muziki, vyakula vya asili, muziki wa kizazi kipya na dini,  tiba asili pamoja na wabunifu wote wa sanaa.

Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dk. Harison Mwakyembe amesema kuwa tamasha hilo ni fursa kubwa ya kutangaza utamaduni wetu, vivutio vya kitalii na kukuza biashara na uchumi wa watanzania katika kila nyanja kama malazi, vyakula na uuzaji wa bidhaa za kitanzania.

“Tamasha hili ni nafasi kubwa ya kutangazia huduma, yakutangaza biashara, bidhaa na fursa nyingi katika nchi yetu, tuna hamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi na mwaka huu litakuwa na mvuto wa kipekee”

Mwakyembe ameongeza kuwa licha ya tamasha hilo kuudhuliwa na wageni na viongozi mbalimbali, litaunganishwa na tuzo za Serengeti inernational film festival kutoa tuzo kwa filamu zenye maudhui ya kiutamaduni na utalii wa mtanzania ambazo zitatolewa usiku wakuamkia kilele na pia kutakuwa na mashindano ya Insha, midahalo na kutembelea vivutio vya utalii hapa Nchini.

 

 

 

 

 

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Machi 21, 2019
Makonda kuwasomesha wanafunzi wa kike 100

Comments

comments