Jeshi la polisi nchini limesema litachukua hatua kali kwa vyuo, shule au taasisi zitakazo bainika kuiuka maelekezo ya kisheria ya kujikinga na kuepuka majanga ya moto.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na msemaji wa jeshi la polisi nchini, David Misime amesema taasisi hizo zinapaswa kufuata kanuni na taratibu zilizopo ili kuepuka madhara ya moto.

Amesema ni wajibu wa kila mmiliki na viongozi wa shule kuendelea kuchukua tahadhari na kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa kutumia wataalam wa masuala ya moto.

Amerejea matukio ya hivi karibuni ya julai 4 na 17 mwkaa huu, kwa shule ya sekondari ya Ilala Islamic kuungua kwa moto na kusababisha vifo vya wanafunzi watatu na uharibifu mkubwa wa maili.

Tukio jingine ni la julai 18, mwaka huu, shule ya sekondari ya Mivumoni Islamic kwa darasa moja kuteketea kwa moto.

“Matukio haya ni wazi kuwa yameleta taharuki na maswali mengi kwa jamii kuhusiana na namna matukio yanavyojitokeza kwa mfululizo, vyombo vya dola vinaendelea kufanya uchunguzi ili kuweza kubaini vyanzo vya moto huo” Amesisitiza Misime

Morrison: Naogopa kupigwa
Mchujo wagombea Ubunge CCM kuanza leo