Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Kangi Lugola amewathibitishia watanzania kulishughulikia kwa haraka na kwa uwezo wa hali ya juu kuhakikisha Mo Dewji anapatikana.

Amewaomba watanzania na wana Dar es salaam kushirikiana na polisi katika kutoa taarifa za kiitelijensia kuhakikisha wote waliohusika na utekaji wa mfanyabaishara huyo wanatiwa mbaroni.

Amesema watu hao wanalitia doa taifa na Rais wetu kwa ujumla.

Lugola amesema hayo kufuatia tukio kubwa lililotokea hapa nchini ambapo watu wasiojulikana alfajiri ya leo wamemteka mfanyabiashara mkubwa Mo Dewji na kumpeleka sehemu zisizojulikana.

Mo ametekwa katika hoteli ya Colosseum ambapo alikwa anaenda kwa ajili ya mazoezi, watu wasiojulikana walifyatua risasi na kumuingiza kwa nguvu katika gari yao.

Aidha kumekuwa na uvumi juu ya kupatikana kwa Mo Dewji jambo ambalo limekanushwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na kusema kuwa bado jeshi la polisi kwa kutumia vyombo vyake vya usalama vitahakikisha Mo anapatikana akiwa salama.

Marekani kusaidia kumtafuta mwandishi wa habari aliyepotea
Spurs kurejea nyumbani Desemba 26

Comments

comments