Mbunge wa Kigoma mjini na Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ametoa ya moyoni mara baada ya kuachiwa huru na jeshi la polisi mkoani Morogoro alipokuwa akishikiliwa kwa tuhuma za kufanya mikutano ya hadhara bila kibali maalumu.

Zitto amesema pamoja na kulazwa selo yeye na viongozi wenzake wataendelea na ziara yao iliyoanza Februari 19, mwaka huu ya kutembelea kata zote ambazo wananchi waliwachagua viongozi kutoka chama hicho kwa malengo ya kushiriki kazi za maendeleo na kuzungumza na kamati za maendeleo za kata hizo.

”Baada ya kulala bure jana polisi Morogoro, tunaendelea na kazi yetu ya kutembelea kata zote ambazo Wananchi walitupa dhamana kwa kuchagua madiwani wa Act Wazalendo”alisema Zitto Kabwe

Zitto ameendelea kufunguka kuwa anasikitishwa na kitendo cha jeshi la polisi  kukamata kamata viongozi na kuwaweka ndani.

Ameita kitendo hiko ni uminywaji wa harakati za kidemokrasia na ukandamizwaji wa sheria na uhuru wa kujieleza.

Aidha ameongezea kuwa ni wajibu wa kila mtu kulinda demokrasia ya vyama vingi na kuimarisha iwe madhubuti kwa ajili ya maendeleao ya watu.

Tusirudishwe nyuma na vitisho, usumbufu na sheria kandamizi. Harakati za kulinda Demokrasia yetu na Uhuru wa kukusanyika, kujieleza na kupashana habari lazima ziendelee. Ni wajibu wetu kulinda Demokrasia ya Vyama vingi na kuiimarisha iwe madhubuti kwa ajili ya Maendeleo ya Watu wetu” amesema Zitto Kabwe.

Pia Zitto ameonyesha kuguswa na muaji mengine ambayo yametokea jana ambapo diwani wa Chadema ameauwa kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali katika mwili wake

Nawapa pole Wananchi wa Ifakara kwa msiba wa Diwani wao aliyekatwa mapanga mpaka kufa jana Usiku. Nilipata taarifa hizo nikiwa selo ya Polisi. Mauaji ya namna hii kwa Viongozi wa kisiasa yanatia doa nchi yetu na ni mwendelezo ya uvunjifu mkubwa wa haki za raia” alisema Zitto Kabwe

Injili ya mchungaji yamtia mbaroni, ''...Wanawake chanzo cha matatizo duniani’'
Mrema amjibu msajili wa vyama vya siasa, ''...hilo ni suala la polisi ''