Chama cha Waandishi wa Habari wanawake Zanzibar (TAMWA-ZNZ), kimemtaka Msajili wa vyama vya siasa Nchini Tanzania Jaji Francis Mutungi kuangalia utaratibu utakaovitaka vyama vya siasa Nchini kubadili vipengele vya katiba za vyama vyao, ili kuleta usawa katika nafasi mbali mbali za uongozi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Chama hicho, Dkt Mzuri Issa, Meneja miradi TAMWA-ZNZ, Ali Mohamed amesema licha ya jitihada mbali mbali zinazoendelea kufanywa na wanaharakati, bado wanawake wengi wameshindwa kupata nafasi za uongozi.

Kazi za makundi kabla ya kuwasilisha sababu wanazoamini zinawakwamisha wanawake wengi Zanzibar kutokua viongozi.

Amesema, ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi ni jambo ambalo limekua likisemewa kwa muda mrefu bila ya mabadiliko, kudai kuwa kitu pekee kilichobaki ni msajili kuvilazimisha vyama vyote Nchini kubadili vipengele kwenye katiba zao.

‘’Naamini iwapo katiba zote za vyama vya siasa vitaweka wazi ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi litakua suala la lazima na ni wazi kuwa kilio cha wanawake cha muda mrefu kitamalizika na hatimae wanawake wengi zaidi watashika hatamu za uongozi,’’ amesema Mohamed.

Mabalozi watakiwa kuainisha fursa za kuinufaisha Tanzania
Aliyekalia kiti cha Rais na aliyeiba kikombe cha kunywea bia wakamatwa