Rais Samia Suluhu Hassan, ameitaka Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU, kufuatilia fedha za UVIKO-19 ambazo zilitolewa kwa ajili ya kushughulikia mambo mbalimbali katika Hifadhi ya Taifa nchini, ambazo haijulikani zilifanya kazi gani.

Rais Samia ameyasema hayo Rais Samia ameyasema hayo hii leo Machi 29, 2023 mara baada ya kupokea ripoti mbili za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na ile ya Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema, “kazi tunayo, CAG nikuombe na hili lifutilie la fedha za TANAPA, nchi hii kama tutasimamia vizuri rasilimali zetu tutaondokana na mikopo labda kama kuna miradi ile ambayo ni mikubwa sana nawaomba sana tufanye kazi.”

Aidha, Rais Samia amebainisha kuwa watendaji wa Serikali wanatakiwa kusimamia vizuri majukumu yao na kuwakumbusha kuwa Taifa la Tanzania ni la wote, hivyo ni muhimu kuwa weledi katika utendaji ili kuleta mabadiliko ya kimaendeleo.

Mbunge Waitara amwaga chozi hadharani, adai ametengwa
Halmashauri 14 zapata hati zenye mashaka, Ushetu yachafuka