Mamlaka ya Hifadhi Nchini (TANAPA) imesitisha shughuli za utalii kwa wageni wote waliopanga kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara hivi karibuni.

Sitisho hilo ni kufuatia daraja la Mto Merera kuvunjika na kusombwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Daraja hilo lipo kilomita moja toka lango kuu la kuingilia hifadhini.

Hivyo Tanapa imewaomba wageni wote waliokuwa wamepanga kutembelea hifadhi ya ziwa hilo kuhairisha safari mpaka pale itakapotoa taarifa juu ya kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo lililosombwa na maji.

 

Video: Mambosasa azungumzia kuhusu kukamatwa kwa Diamond, Nandy, Bill Nas na Hamissa Mobeto
Mwinyi alia na amani ya nchi

Comments

comments