Kila mtu amekuwa na mtazamo tofauti juu ya suala la Tanasha Dona ambaye kwa sasa ni mpenzi wa Diamond Platinumz kukutana rasmi na familia ya mwanamuziki huyo anayefanya vizuri hapa nchini.

Wengi wamekuwa na mtazamo hasi hasa kwa upande wa familia ya Diamond Platinumz wakisema kuwa imekuwa kawaida kwa familia hiyo kupokea kila aina ya mwanamke aneyeletwa na Diamond.

Dada wa Diamond al-maarufu kama Esma amewahi kusikika akisema kuwa alipo kaka yake naye yumo akimaanisha kuwa jambo lolote analofanya kaka yake anamuunga mkono.

Vivyo hivyo mama wa Diamond, Bi Sandra naye amewahi kusikika akiwaambia mashabiki wa familia hiyo kuwa waache kufuatilia mambo ya familia yake wafuatilie mambo ya familia zao.

Tafsiri hiyo inamaanisha kuwa familia nzima ya Diamond ipo pamoja na Diamond na wapo tayari kuunga mkono chochote kitu kinachofanywa na msanii huyu au ndugu yao huyo.

Ijapokuwa mashabiki wameoneshwa kukerwa na kitendo cha mama Dangote kukubaliana na kila jambo linalofanywa na mwanae Diamond Platinumz wakidai kuwa kama mama lazima awe na mipaka na kijana wake na sio kila mwanamke wake anamleta kumtambulisha kwani kama mzazi na suala zima la malezi haileti picha nzuri na mfano mzuri wa kuigwa kama kioo cha jamii.

Aidha Diamond amewahi kuwa na warembo tofauti tofauti ambao wote tayari wameshatambulishwa katika familia hiyo, akiwemo Wema Sepetu, Zarinah Hassan, Hamisa Mobetto na wengine ambao bado hawajafahamika.

Na katika orodha hiyo Diamond alifanikiwa kuzaa na wanawake wawili tuu ambao ni Zari pamoja na Hamissa Mobeto.

Nini maoni yako kama mzazi, kijana ambaye unataka kujifunza kitu kutoka kwa msanii huyu mkubwa anayefanya vizuri katika tasnia ya muziki hapa nchini na ukizingatia hivi karibuni ametangaza kufunga ndoa na mtangazaji huyo wa redio huko nchini Kenya, Tanasha Donna.

Jaji Nsekela awatahadharisha viongozi wa umma
Watawa, Wanakijiji watakiwa kutumia busara kumaliza mgogoro wa ardhi

Comments

comments