Wakazi wa Tandale Uzuri wilayani  kinondoni wamelalamikia jeshi la polisi nchini kwa kushindwa kuwadhibiti vijana wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu, vikiwamo vya ubakaji na uporaji.

Vijana wanaokaa katika vituo vya daladala na vichochoro vya mitaa mbalimbali wakiwavizia wananchi wanaokuwa ndani ya magari na wanaopita mitaani na kuwapora mali zao. Mkazi wa eneo hilo Bakari Idd alisema limekuwa suala la kawaida katika eneo hilo kushuhudia wahalifu hao wakiwaibia wananchi mali zao bila kuchukuliwa hatua kwani kituo cha polisi hakipo mbali na eneo hilo.

“Watu wa hapa wanamazoea kuna wakati unashuhudia mtu akikabwa lakini unashindwa kumsaidia, kwani vijana hawa wako makundi na wanaweza kukudhuru ,” alisema.

Alisema wengi wao  wanapofanya uhalifu na kuuza vitu walivyoviiba hununua dawa za kulevya na zinapowaishia hurudi tena vituoni na mtaani kuendeleza uhalifu.

Hivyo waliliomba jeshi la polisi lisaidie katika kukomesha hali hii mtaani hapo,  kuwakamata na kuwafikisha mahakamani ili usalama urejee katika eneo hilo.

 

 

 

 

Video: Rais wa Colombia atangazwa mshindi tuzo ya amani ya Nobel 2016
Ndalichako awaadhiibu vikali walimu wa mafunzo waliohusika na kipigo cha mwanafunzi mbeya.