Hali si shwari ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), baada ya wakurugenzi watatu wa Shirika hilo kushushwa vyeo huku mwingine akiacha kazi mwenyewe.

Tukio hilo limekuja mara baada ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Felchesmi Mramba na siku moja baada ya kuanza kazi kwa Dkt. Tito Mwinuka aliyeteuliwa kukaimu nafasi hiyo.

Aidha, wakurugenzi  watatu wamehamishiwa katika chuo cha Tanesco(TTS) kilichoko eneo la karibu na stesheni ya Kampuni ya Reli Tanzania(TRL), jijini Dar es salaam.

“Sina mengi ya kueleza kuhusu hilo. kwa taarifa zaidi naomba uwasiliane na msemaji wa Tanesco kwaajili ya ufafanuzi zaidi,”amesema Dk. Kyaruzi.

Walioshushwa vyeo ni Naibu Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Shirika hilo, Decklan Mhaiki,aliyekuwa Mkurugenzi wa Usambazaji, Sophia Mgonja na Johari Kachwamba wakati aliyekuwa Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu Watson Mwakyusa akiamua kuacha kazi.

Ridhiwani: Vijana hudhurieni mikutano ya vijiji
Kambi ya Rais Mteule wa Gambia yanena kuhusu taarifa za kupigwa risasi