Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limekamisha ahadi ya Rais John Magufuli ya kufikisha umeme katika kiwanda cha juice kilichoko wilaya ya Mkurunga, mali ya mfanyabiashara Said Bakhresa.

Rais Magufuli alitoa agizo hilo alipotembelea kiwanda hicho. Aliagiza Tanesco kuhakikisha umeme unaunganishwa kwenye kiwanda hicho ndani ya kipindi cha miezi miwili.

Mkurugenzi Mtendaji wa wa Tanesco, Felchesmi Mramba jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa shirika hilo lilikamilisha agizo hilo tangu Novemba 30 mwaka huu.

Mramba ameeleza kuwa shirika hilo limekamilisha kazi yake lakini halikuweza kuunganisha moja kwa moja kwenye kiwanda hicho kwakuwa bado mfanyabiashara huyo hajakamilisha kuweka miundombinu.

Alisema tayari Bakhresa ameagiza vifaa vinavyohusika ili kukamisha zoezi hilo. Kiwanda hicho kinatarajia kuwa msaada mkubwa kwa kilimo cha matunda nchini pamoja na kuongeza nafasi za ajira kwa watanzania wengi.

Lowassa: Fidel Castro ni shujaa wangu wa dunia
Magufuli afanya mabadiliko ndani ya CCM