Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk Tito Mwinuka amekanusha tetesi zinazodai kupanda kwa bei ya umeme nchini amesema kuwa wao hawawezi kupandisha bei ya umeme kwani bei iliyopo tayari imepitishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji, (Ewura).

Tetesi hiyo ni kufuatia tozo ya 1.1% wanayokatwa wateja baada ya kununua umeme kwa njia ya mitandao ya simu, utaratibu ambao umeanza kufuatwa Aprili 2, mwaka huu mara baada ya Tanesco kuunganisha mifumo ya malipo na ule wa Serikali wa GeGP ambao utawalazimu wateja kulipia gharama za miamala ya kununua umeme.

Tofauti na hapo awali ambapo huduma ya kununua umeme kwa njia ya simu ilikuwa inatolewa bure kwa wateja.

Hivyo Meneja masoko wa Tanesco amearifu umma kuwa kukwepa gharama hizo na kuendelea na utaratibu wa awali wa kununua umeme bila makato yeyote, wateja watalazimika kulipia au kununua umeme katika ofisi za Tanesco, Benki ya NMB au CRDB.

Aidha ametoa ufafanuzi na kueleza kuwa endapo mteja atanunua umeme kwa njia ya simu makato yake yatakuwa kama yafuatavyo, umeme wa 5,000, mteja atachangia sh55, huku umeme wa 10,000 mteja atachangia 110, na umeme wa 100,000 mteja atachangia 1,100 ambayo ni sawa na asilimia 1.1.

 

Video: Rais Magufuli ampa milioni 100 mzee aliyegundua Madini ya Tanzanite
Ligi kuu kuendelea leo