Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), limetoa tamko kufuatia agizo la Rais John Magufuli la kutoendelea na mikataba kati yake na makampni ya kufua umeme nchini, aliyoeleza kuwa inaliingizia Taifa gharama kubwa zisizokuwa na lazima.

Tanesco imeshatumia takribani shilingi trilioni 4.6 kwa ajili ya kuyalipa makampuni yenye mitambo ya kufua umeme nchini kama gharama za uwekezaji (capacity charge), likiwemo kampuni ya IPTL/PAP iliyozaa mgogoro uliozua sakata la Escrow.

Mkurugenzi mtendaji wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema kuwa baada ya muda mfupi hakutakuwa tena na mikataba ya aina hiyo ikiwa ni sehemu ya kutekeleza agizo la Rais Magufuli. Alisema kuwa tayari Shirika hilo limeshamaliza mkataba na kampuni moya ya kufua umeme na kwamba baada ya mwezi mmoja kampuni nyingine itamaliza mkataba wake.

Juzi, Rais Maguli alizindua mradi wa mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi II, na kueleza kuwa nchi inatakiwa kuwa na mitambo yake badala ya kukodi kutoka kwa makampuni ambayo inachaji gharama kubwa zaidi.

“Tuachane na mitambo ya kukodi. Tumechoka kufanyishwa biashara na makampuni ya uwekezaji. Tujenge mitambo yetu wenyewe. Tunalipa capacity charge za ajabu ajabu halafu tunalipia gharama ya ajabu,” alisema Rais Magufuli.

 

 

Wachezaji Wa Simba Wajazwa Fedha Kwa Ushindi Mfululizo
Simba Kujenga Uwanja Kwa Fedha Za Emmanuel Okwi