Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) linawataarifu wateja wake wa Ilala Tol na Ilala Kurasini kuwa kutakuwa na shida ya umeme kwa maeneo hayo kutokana na hitilafu iliyojitokeza mara baada ya lori kubwa kugonga nguzo eneo la puma.

Kufuatia hitilafu hiyo baadhi ya maeneo yataathirika kwa kukosa umeme, maeneo hayo yametajwa kuwa ni Mwakalinga road, Duce, Keko, , Temeke, Changombe yote, Jamana printers, Quality plaza, Viwanda base, Tanzania oxygen, Azania, JKT, Uwanja wa taifa, Kurasini yote, Uhamiaji, Unifreight, Twalipo, Bandari, Transcargo, Malawi cargo baraza la maaskofu, Dockyard, Uhasibu, Mtoni kijichi, Kata za Vijibweni, Tungi, Kigamboni, Mjimwema, Somangila, Kimbiji na Pembamnazi na maeneo jirani.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza na kutoa tahadhali kwa wananchi wa maeneo hayo kuwa wasishike waya uliokatika hivyo uangalizi uwe mkubwa hasa kwa watoto.

Kwa taarifa zaidi imetoa namba za mawasiliano, Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

 

Mtindo wa maisha usiokatisha ndoto zako
Ummy awatoa hofu watanzania juu ya Ebola