Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa semina maalumu ya matumizi bora na usalama wa umeme kwa Taasisi ya Maendeleo kwa Viziwi (TAMAVITA) ili kuliwezesha kundi hilo kutambua umuhimu wa Nishati ya Umeme na mazingira hatarishi kwa mtumiaji wa Umeme.

Akizungumza wakati wa utoaji semina hiyo jijini Mwanza, Meneja Mwandamizi wa Kanda ya Ziwa ambaye amemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi Maclean Mbonile amesema kuwa TANESCO imeona ni vyema kuungana na kundi hilo maalumu ili kuwapatia elimu inayohusu masuala mbalimbali ya umeme .

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dkt. Severine Larika amelipongeza shirika hilo kwa kuwatambua watu hao ambapo amesema kuwa mara nyingi husahaulika katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Aidha, Jumla ya walemavu 30 na viongozi wao kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza wamenufaika na elimu hiyo ambao nao kimsingi wataisambaza kwa wengine.

Mbunge amwaga fedha ujenzi wa vyumba vya madarasa
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Machi 8, 2019