Ofisi ya Jeshi la Polisi iliyopo mji mdogo wa Himo wilaya ya Moshi mkoa wa Kilimanjaro imekatiwa umeme na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoani humo kutokana na madai ya malimbikizo ya deni la zaidi ya Sh. bilioni tatu.

Hatua hiyo imetokana na operesheni ya kusitisha kutoa huduma ya umeme katika taasisi mbalimbali za serikali ambazo zimekuwa zikidaiwa kwa muda mrefu.

Aidha, kwa upande wake Meneja wa Tanesco Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Mahawa Mkaka, amesema kuwa operesheni hiyo ni maalumu kwa ajili ya kuwakatia umeme wadaiwa sugu wanaoongoza wakiwamo polisi, Jeshi la Magereza, hospitali za serikali, Mamlaka za Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika Wilaya za Same na Mwanga.

“Shirika litaanza kusitisha huduma ya umeme katika taasisi hizo mara moja kutokana na kushindwa kulipa madeni yao kwa wakati na kuisababishia mamlaka hiyo kushindwa kujiendesha kwa ufanisi na kuboresha huduma zake kwa wananchi,” amesema Mkaka.

Hata hivyo, ameongeza kuwa shirika hilo limetoa ofa maalumu ya punguzo kwa kipindi hiki endapo mteja anayedaiwa atalipia deni lake na kwamba atasamehewa gharama za riba zinazoongezeka kutokana na kulimbikiza madeni kwa muda mrefu.

 

Alphonso Davies aweka rekodi MLS
Simiyu: Tunaweza vipi kusema NASA bado ipo?