Uongozi wa mkoa wa Tanga umeweza kuwa mfano kitaifa katika utekelezaji wa miradi kwa njia ya ‘Force Account’ kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na kukamilisha kwa muda mfupi.

‘Force Account ni mfumo unaohusisha matumizi ya fedha kidogo kwa matokeo makubwa ikiwa ni pamoja na ununzi wa vifaa vya mradi moja kwa moja, kutumia mafundi wa kawaida na kuwasimamia kwa kutumia wataalamu wa ndani (RS).

Mkoa wa tanga umefanikiwa kukarabati makazi ya viongozi wa mkoa huo, ofisi za maafisa tarafa 24, samabamba na miradi mingine ya elimu, afya na miundombinu mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya Tsh. bilioni tatu.

 

Samatta kucheza fainali ya Carabao na Manchester?
DSTV yaja na ofa, kwa 29,000 tu, unaweza kutazama ligi zote Uingereza