Chama Cha Wauguzi Nchini (TANNA) kimelaani tukio la shambulio la muuguzi lililotokea tarehe 18, Februari 2018 katika Hosptali ya Bugando jijini Mwanza na ndugu wa mgonjwa ambaye muuguzi huyo alikuwa akimuhudumia na kufariki dunia.

Makamu wa Rais wa Chama cha Wauuguzi nchini Dk. Ibrahim Mgoo, amesema kuwa kabla ya shambulio hilo muuguzi alitimiza wajibu wake wa kazi , alishambuliwa na watu wanaojulikana wiliokuwa na kusudi la kutoa uhai katika chumba cha uangalizi maalumu (HDU), Hospitalini hapo, ambapo ni kinyume na taratibu za hosptali hiyo.

“Kabla ya mauti kumfika mgonjwa huyo ndugu zake walilazimisha wabaki katika chumba hicho jambo ambalo, halikukubaliwa na muuguzi huyo, kesho yake walipotaarifiwa ndugu yao amefariki, ndipo walipoamua kufanya kitendo cha unyama na udhalilishaji kwa kumshambulia na kumjeruhi muuguzi alipokuwa anatoa huduma kwa wagonjwa wengine”, alisema.

Makamu Mgoo, ameviomba vyombo vinavyohusika kuchukua hatua stahiki, kwa wahusika mapema ili kutoathiri utendaji wa wauguzi nchini, ikiwa ni pamoja na kuboresha ulinzi wa wauguzi na watumishi wengine mahala pa kazi ili kutoleta madhara makubwa katika kazi.

Aidha, ametoa shukrani kwa hatua zilizochukuliwa na uongozi wa Hospitali ya Bugando ukishirikiana na chama cha wauguzi, kuhakikisha Muuguzi huyo anatendewa haki katika vyombo vinavyohusika.

Video: Musiba kuburuzwa kortini
Twaweza: 38% ya watoto hawajui kufanya majaribio ya darasa la pili