Shirika la Afya Duniani, WHO limetangaza mpango wa muda kuhusu jinsi nchi zitakavyopewa chanjo za corona mwaka huu, huku Tanzania na Burundi zikiwa hazimo.

WHO imesema kuwa chanjo hizo ambazo ni dozi milioni 336 za AstraZeneca/Oxford na Pfizer-BioNTech, zitatolewa kwa muhula wa kwanza na wa pili wa mwaka 2021.

Katika awamu hii, nchi zitapewa kwa sawa na 3.3% ya watu katika kila nchi katika mpango huu, kulingana na malengo ya shirikisho la chanjo duniani (GAVI) ya utoaji wa chanjo kwa 3% ya wakazi wa dunia katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka 2021.

Wiki iliyopita Rais John Pombe Magufuli aliwatahadharisha viongozi kutopokea chanjo za corona ambazo alisema zinaweza kuleta athari kwa raia.

Baada ya kuongezeka kwa idadi ya maambukizi ya Covid, hivi karibuni serikali ya Burundi ilitangaza mkakati mpya wa kupambana na Covid-19, ikiwa ni pamoja na kufunga mipaka ya majini na nchi kavu na uvaaji wa barakoa katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu.

Msolla: Tambwe atalipwa kwa utaratibu tuliojiwekea
PICHA: Waziri wa michezo atembelea Azam Complex