Msemaji wa Serikali ya Tanzania, DkT. Hassan Abbas amesema nchi haiwezi kusema haina au haijawahi kupata mgonjwa wa corona kwa sababu ni sehemu ya dunia na kuna mwingiliano wa watu kutoka mataifa mbalimbali.

Amesema kuwa licha ya Tanzania kufanikiwa kuudhibiti ugonjwa huo amekiri kuwa wakati mwingine wagonjwa wa corona hugundulika hususani raia wa kigeni wanapoingia nchini.

Ameeleza hayo wakati akihojiwa na mtangazaji Salim Kikeke wa Televisheni ya BBC Swahili.

Dkt. Abbas amesema mapambano ya ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya corona yamefanikiwa kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kisayansi na asili huku Serikali ikiwa makini  kudhibiti ugonjwa huo tangu mapema.

Mawakili wa Trump kupanga hoja
Magufuli: Abood umeua viwanda