Mgombea uras kwa tiketi ya ACT – Wazalendo, Bi. Anna Mghwira amesema kuwa Tanzania imekosa viongozi bora wanaoweza kuiletea maendeleo makubwa licha ya kuwa na utajiri mubwa wa maliasili.

Bi. Mgwira ameyasema hayo katika mkutano wa kampeni aliofanya katika mjini Katavi hivi karibuni. Aliwataka watanzania kuhakikisha wanaitumia fursa ya kupiga kura ifikapo October 25 mwaka huu na kuwatowarusha madarakani viongozi walewale walioshindwa kuwaletea maendeleo kwa kipindi cha zaidi ya miaka 50.

“Watu wanaojua na wanaoguswa na matatizo ya watu ndio wanaopaswa kuliongoza taifahili ambalo kwa miaka 50 limekuwa likiburuzwa na viongozi ambao wanajigamba kuwa wamelibadili kwa maisha bora,” alisema huku akiwataka wananchi hao kumchagua yeye na chama chake ili kuleta mabadiliko ya kweli.

Aliahidi wananchi hao kuwa endapo watampa ridhaa ya kuiongoza Tanzania atahakikisha wananchi wa Katavi wanapata ajira kutokana na misitu ya eneo hilo.

Tanzia: Asley Wa Yamoto Band Ampoteza Mama Yake Mzazi
Mkuu Wa Majeshi Anusurika Kuuawa