Serikali ya Tanzania na Kenya  zimeweka mikakati ya makubaliano ya mfumo wa kufanya kazi kwa pamoja katika kujadili na kuweka mapendekezo kwenye sekta ya utalii ili kuhakikisha inaimarika na kufikia ngazi ya Kimataif.

Akizungumza katika mkutano wa ushirikiano wa masuala ya utalii baina ya nchi hizo Jijini Arusha leo Septemba 25, 2021 ,Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Tanzania,Dkt.Damas Ndumbaro amesema mfumo huo utafanya kazi ya kujadili pamoja na kuweka mapendekezo mwishoni kupitishwa na Mawaziri wa sekta hiyo Kenya na Tanzania kwa ajili kusonga mbele.

Aidha Waziri Ndumbaro amesema kuwa  Sekta ya utalii ni  muhimu sana kwa Kenya na Tanzania kwasababu inatoa mchango mkubwa katika uchumi wa nchi zote mbili  kwani kabla ya uviko -19 nchini Tanzania utalii na misitu ilikuwa inachangia asilimia 21.5 ya uchumi wa nchi pia ilikuwa inachangia asilimia 25 ya fedha za kigeni.

“Utalii na Misitu ilikuwa inatoa ajira takribani milioni sita kwa hiyo ni sekta muhimu kwa kuwa tunaamini kwamba bado hatujafikia  pale tanapaswa kufikia na ili kuweza kufikia yatufaa tuongeze ushirikiano na majirani zetu ili tuweze kukuza utalii wetu,” Amesema Waziri Nbumbaro.

Waziri Ndumbaro amesema maamuzi ya mawaziri sita nikufanya onyesho hilo kuwa kubwa zaidi duniani na onyesho lingine litafanyika mwakani nchini Burundi lengo ikiwa ni kuleta wadau wote duniani waweze kutembelea nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa heshima ya pili waliipata nchini Cape Vede ambapo UNWTO iliiteua Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa 65.

Kwa upande wake Wziri wa Utalii na wanyamapori  wa Kenya,Najibu Balala amesema nchi hizo mbili zimekubaliana kushirikiana hali ambayo itasaidia kuvuta watalii hapa nchini pamoja na nchi ya Kenya kwani ni jamii moja hata mbuga za wanyama pia zimewaunganisha.

Ikumbukwe kuwa hatua hii ya kukutana na kufanya mkutano kati ya Waziri wa Utalii wa Maliasili na Utalii wa Tanzania na Waziri wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya ni  hatua ya utekelezaji wa kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili mara baada ya uhusiano huo kudorora kwa muda mrefu hali iliyomlazimu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani mara tu baada ya kuapishwa kufanya ziara ya nchini Kenya ambapo alifanya mazungumzo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo majirani.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akimkabidhi zawadi mbalimbali kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) Waziri wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya, Najib Balala (kushoto) mara baada ya  mkutano uliofanyika leo Jijini Arusha wenye lengo  wa kuimarisha  ushirikiano katika masuala ya utalii baina ya nchi ya Tanzania na Kenya ambapo katika mkutano huo   wamekubaliana kuweka mkakati wa kufanya kazi kwa pamoja katika masuala  ya utalii
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akimkabidhiwa zawadi mbalimbali ikiwemo kofia aliyoivaa kutoka kwa  Waziri wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya, Mhe. Najib Balala (kushoto) mara baada ya  mkutano uliofanyika leo Jijini Arusha wenye lengo  wa kuimarisha  ushirikiano katika masuala ya utalii baina ya nchi ya Tanzania na Kenya ambapo katika mkutano huo   wamekubaliana kuweka mkakati wa kufanya kazi kwa pamoja katika masuala  ya utalii
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akivishwa ‘badge’ ya Shirika la Wanyamapori la Kenya ikiwa ni miongoni mwa zawadi mbalimbali alizopewa na  Waziri wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya, Mhe. Najib Balala (kushoto) mara baada ya  mkutano uliofanyika leo Jijini Arusha wenye lengo  wa kuimarisha  ushirikiano katika masuala ya utalii baina ya nchi ya Tanzania na Kenya ambapo katika mkutano huo   wamekubaliana kuweka mkakati wa kufanya kazi kwa pamoja katika masuala  ya utalii
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akimkabidhi zawadi mbalimbali kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) Katibu Mkuu wa  Utalii na Wanyamapori wa Kenya, Safia Kwaka (kushoto) mara baada ya  mkutano uliofanyika leo Jijini Arusha wenye lengo  wa kuimarisha  ushirikiano katika masuala ya utalii baina ya nchi ya Tanzania na Kenya ambapo katika mkutano huo   wamekubaliana kuweka mkakati wa kufanya kazi kwa pamoja katika masuala  ya utalii

Habari Picha: Rais samia alivyowasili Nchini
Bilioni 11 kukarabati uwanja wa ndege Arusha