Tanzania ni kati ya nchi tano Barani Afrika na pia ni nchi pekee ya Afrika Mashariki inayozalisha mionzi dawa.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Gwodin Mollel ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Maabara ya Afya ya Jamii iliyoko katika hospitali ya Magonjwa Ambukizi ya Kibong’oto iliyofunguliwa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango.

Amesema, hatua hiyo inatokana na uwekezaji mkubwa wa vifaa tiba uliofanywa na Serikali.

Vyumba vya kuttolea matibabu, Kibongoto Hospital, Siha Kilimanjaro.

Dkt. Mollel amesema, uwekezaji huo umeifanya Tanzania kuwa na uwezo wa kupasua vivimbe vya ubongo bila kupasua kichwa na hivyo kupunguza gharama kwa Serikali ambazo ilikua inazipata kwa kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi.

Kwa upande wa kupandikiza uloto Dkt. Mollel alisema kwa mgonjwa mmoja nje ya nchi Serikali ilikua ikilipa Milioni 250, lakini kwa sasa hapa nchini upandikizaji huo utagharimu Milioni 70 na kufanya uokoaji wa shilingi Milioni 180.

Upasuaji wa vivimbe vya ubongo kwa nje ya nchi kwa mgonjwa mmoja ilikua ikigharimu Milioni 90 lakini kwa hapa nchini zoezi hilo linafanyika kwa Milioni 8.

Wahudumu wa Afya waaswa maadili ya kazi
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Julai 18, 2022