Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaongoza kwa kushtakiwa katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu (AfCHPR).

Mahakama hiyo ina kesi 180 ambapo kati ya hizo 117 zimefunguliwa dhidi ya Serikali huku 94 kati ya 117 zikiwa zimefunguliwa na wafungwa na mahabusu waliopo magereza.

Hayo yamesemwa Jijini Arusha katika kikao kilichowakutanisha Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Julius Mashamba, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi pamoja na Msajili wa Mahakama ya Afrika, Dkt. Robert Eno, ambapo Wakili Dkt. Mashamba amesema kuwa ofisi yake iliona haja ya kutembelea mahakama hiyo mbali ya kujifunza lakini pia kuona uendeshaji wa shughuli zake.

“Kwa taarifa walizotupatia hadi sasa Tanzania ndiyo nchi inayoongoza kwa kushtakiwa ikiwa na kesi 117. Tumegundua wengi walioishtaki Serikali kuhusu haki zao ni watu waliopo gerezani au mahabusu,” amesema Dkt. Mashamba

Aidha, Dkt. Mashamba amesema kuwa wamejaribu kuieleza Mahakama ya Afrika nia ya Serikali ya kutaka kuona haki za kila mtu zinalindwa na pale wananchi wanapoona haja ya kwenda mahamakani basi Serikali pia ipate fursa ya kujitetea.

Hata hivyo,ameongeza jambo kuwa lililowafanya pia watembelee mahakama hiyo ni wingi wa kesi hizo na hasa zikichukuliwa kuwa zimekuwa zikifanana kwani wengi hudai kutopata msaada wa kisheria wakati mahakama za ndani zilishatoa uamuzi wake.

 

Zidane huenda akajiunga na Manchester United
VIDEO: Samatta azungumzia ’’Hat Trick’’ aliyofunga hivi karibuni.