Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo amesema katika Mkutano 27 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP27), Tanzania imekuwa ni nchi kinara katika uandaaji wa Mwongozo wa Biashara ya Hewa ya Ukaa.

Waziri Jafo, amesema hayo hii leo Novemba 12, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini China na Misri hivi karibuni.

Amesema, “hapo mwanzo hatukuwa na kanuni wala mwongozo wa biashara hii na hivi sasa kukamilika kwake kutasaidia Tanzania kuweza kupata rasilimali fedha za kupambana na mabadiliko ya tabianchi.”

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo.

Ameongeza kuwa, “Ni kweli changamoto ya uzalishaji wa hewa ukaa ni kubwa na nchi yoyote dunia inapofanya uchafuzi huo wa hewa zinaathrika nchi zote duniani na ndio maana wataalamu wanatuambia ifikapo mwaka 2050 kuna uwezekano barafa katika mabara mbalimbali katika milima ukiwemo Kilimanjaro zitayeyuka kutokana na ongezeko la joto.”

Aidha, Waziri Jafo ameongeza kuwa, kutokana na hali hiyo Mkutano wa Paris wa mwaka 1992 uliazimia nchi zinazoendelea ambao ndio wazalishaji wakubwa wa hewa ukaa wanapaswa kuchangia zaidi ya Dola za Marekani bilioni 100 kwa nchi zinazoendelea kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

Picha: Mafanikio ya ziara ya Rais nchini China na Misri
Samia aongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM