Serikali nchini, inaendelea kuhakikisha kuwa inaweka mazingira wezeshi ambayo yanawawezesha wafanyabiashara, wawekezaji na wadau wote wa taasisi binafsi kuweza kufanya biashara na uwekezaji katika Mkoa wa Pwani.

Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Pwani kutoka Idara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Rehema Akida ameyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na Maafisa Habari wa Idara ya Habari – MAELEZO, kuhusu uwekezaji wa viwanda uliopo katika mkoa huo.

Amesema, “Vivutio vya wawekezaji Pwani ni kuwa karibu na masoko likiwemo la Dar es Salaam, miundombinu ya barabara ya kufikia masoko ya ndani, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Afrika Mashariki, uwepo wa miundombinu katika maeneo ya uwekezaji pamoja na uwepo wa kituo cha huduma za pamoja kinachowasaidia kupata huduma zinazohitajika kiurahisi.”

Aidha, Akida ameongeza kuwa, mkoa huo umekuwa na maendeleo makubwa katika sekta ya viwanda ambapo kwa mwaka 2021, mkoa ulikuwa na viwanda 1,453 na katika kipindi cha miaka miwili mkoa umeweza kuwa na viwanda 1,522 ongezeko la viwanda 69 vikiwemo vikubwa 27 na vidogo 94 na vingine vingi vidogo.

Amesema, mkoa huo una viwanda vya aina mbalimbali vikiwemo vikubwa tisa vya kutengeneza na kuunganisha magari, 17 vya kuchakata mazao ya kilimo, kiwanda kikubwa cha sukari cha Bagamoyo, viwanda vinavyohusika na utengenezaji wa nguzo za umeme za zege na 14 vya kuchakata mazao ya mifugo na ngozi.

Uwepo wa viwanda mkoani Pwani umekuwa na manufaa kwa kutoa ajira hivyo kukuza kipato na uchumi wa mwananchi mmoja mmoja ambapo kwa miaka miwili hii, jumla ya ajira 17,659 za moja kwa moja na 50,000 zisizo za moja kwa moja zilipatikana, kuongezeka kwa mchango mkubwa wa viwanda katika Pato la Taifa.

Fei Toto afunguka kwa mara ya kwanza
Rubani afichua madhaifu ajali ya Ndege