Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa Makala ya Tanzania itakayorushwa katika kipindi maarufu Duniani Royal Tour kitasaidia kuitangaza vizuri Tanzania.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Rais Samia amesema pia kupitia makala hiyo utalii unakwenda kuinuka lakini pia kuvutia wafanyabiashara, wawekezaji na kuondoa upotoshaji wa makusudi kuhusu Tanzania.

Akizungumza na Dar24Media kupitia kipindi cha mahojiano mchambuzi wa masuala ya Kisiasa na kijamii Said Miraji, amesema kuwa Royal Tour ni kipindi cha Kimatafa ambapo mataifa mbalimbali yataangalia na kujua utalii wa Tanzania, pia itasaidia mataifa kujua madini ya Tanzanite yanatokea Tanzania.

Amesema kuwa kupitia makala hiyo milango ya fursa za kibiashara na uwekezaji zitaongezeka lakini pia hata kukuza sanaa ya Tanzania.

Nabi: Tunatakiwa kuwafunga Rivers United mabao mengi
Hitimana Thiery kumbe amekwenda shule!