Tanzania inaweza kufikia Uchumi wa Kipato cha Juu hivi karibuni, baada ya kufikia Uchumi wa Kipato cha Kati wiki chache zilizopita kutokana na mafanikio makubwa yanayoonekana hususan kwenye  sekta ya madini nchini, Dar24 Media inaripoti.

Sekta ya madini imefanikiwa kuvunja rekodi ya miaka minne, baada ya kurekodi mapato ya zaidi ya Sh. 358.9 Bilioni, kutoka kiwango cha wastani wa Sh. 196 Bilioni zilizokuwa zinapatikana kwa kipindi cha miaka minne iliyopita.

Hatua hiyo imefikiwa kutokana na juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kudhibiti na kuboresha sekta hiyo, ikiwa ni pamoja na kujenga ukuta kuzunguka Mgodi wa Mirerani ambao ndilo eneo pekee duniani linalozalisha madini ya Tanzanite.

Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (Tamida), Sammy Mollel amewataka wafanyabiashara wa madini kujikita katika kununua mashine za kisasa zinazoweza kuongeza thamani zaidi kwenye bidhaa za madini.

“Tunawashauri wafanyabiashara na wadau wengine kununua mashine zaidi ili tuweze kuongeza thamani ya madini ambayo itamaanisha kuongeza fursa za ajira na pato la taifa,” Mollel amekaririwa na Daily News.

“Rais Magufuli amefanya kazi nzuri sana kiasi kwamba ni vigumu hata kutaja zote, amekuwa kiongozi wa mfano sio tu hapa nchini bali pia Afrika na mataifa mengine duniani,” ameongeza.

Amesema kuwa Serikali imefanikiwa kuondoa ubadhirifu na kuziba mianya ya rushwa, kazi iliyofanywa vizuri na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na vyombo vingine.

Tanzania kufika Uchumi wa Juu, sekta ya madini yavunja rekodi ya miaka 4

Marufuku ya uuzaji wa pombe Afrika Kusini yarejea kukabili Corona

Mgonjwa wa kwanza wa corona aidai Serikali 'mamilioni' - Kenya
Marufuku ya uuzaji wa pombe Afrika Kusini yarejea kukabili Corona