Ni rasmi sasa Tanzania itawakilishwa na klabu  nne kwenye michuano ya klabu Barani Afrika kuanzia msimu ujao 2021/22, baada ya klabu ya ASC Jaraaf ya Senegal kutolewa kwenye mashindano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.

ASC Jaraaf ilitolewa kwa faida ya bao la ugenini dhidi ya Coton Sport ya Cameroon, baada ya kufungwa 1-0 kwa sifuri katika mchezo wa mkondo wa kwanza, na jana ilishinda 2-1 nyumbani.

Kuondolewa kwa klabu hiyo kunaifanya Senegal kubali na alama 15 huku Tanzania ikiwa na alama 27.5, katika orodha ya Shirikisho la soka BArani Afrika CAF.

Tanzania imejiongezea alama kwenye msimamo huo, kufuatia kufanya vyema kwa mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC msimu huu 2020/21, na kuondolewa hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa kufungwa jumla ya mabao 4-3 dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Tanzania itaingiza timu mbili kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, na klabu nyingine mbili zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Hiyo itakua ni mara ya pili kwa Tanzania kuingia timu nne kwenye michuano ya klabu Barani Afrika, mara ya kwanza ilikua msimu wa 2019/20 ambapo upande wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika timu shiriki zilikuwa Simba SC na Young Africans, na upande wa Kombe la Shirikisho zilikwenda Azam FC na KMC FC.

Wabunge wapya waapishwa
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Mei 24, 2021