Vifo vya watoto wachanga wenye umri wa mwaka 1-15 vimepungua kutoka 147 1999 hadi kufikia 67 kwa 2015, ambapo kumewezesha serikali kutimiza lengo la Nne (4) katika yaliyokuwa Malengo ya Millenia ya 2015.
Katika uzinduzi wa ripoti ya utafiti maalumu wa afya ya uzazi,mtoto na malaria uliofanywa na ofisi ya takwimu taifa NBS kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa afya leo jijini Dar es salaam, Dk. Mpoki Ulisubisya amesema matokeo hayo yachukuliwe kama chachu ya kitaifa ili kuendelea kuboresha afya.
Kabla ya kuzindua ripoti hiyo ambayo ni ya sita kufanyika nchini Katibu Mkuu Wizara ya afya maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Dk. Mpoki Ulisubisya amewataka wananchi wote nchini kutumia vyandarua vinavyotolewa na serikali na si kufanyia matumizi mengine kama jinsi ambavyo huwa inaonekana.
Aidha katika hatua nyingine ameongeza kwamba ongezeko la mabinti wadogo ambao huacha shule kwa kubeba mimba ni kuchochea ongezeko la umasikini nchini ikiwa ni pamoja na Taifa kukosa wasomi na wakati mwingine hao watoto wanaozaliwa hufariki pia.
Pamoja na hayo Dk. Ulisubisya amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kutoa elimu juu ya madhara yanayoweza kutokea kwa wasichana kuzaa wakiwa bado wadogo, na kuongeza kuwa serikali ina nia ya makusudi ya kuhakikisha sheria ya Ndoa inafanyiwa marejeo ili kuhakikisha baadhi ya changamoto hizo zinashughilikiwa
Hata hivyo jumla ya wauguzi 66 walitembelea kaya zote nchini ili kukusanya takwimu za utafiti huu ambapo ulianza rasmi mwezi wa nane 2015 hata hivyo ripoti kamili inatarajiwa kutoka rasmi ifikapo octoba.2016.