Norway, imeihakikishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ushirikiano katika sekta za kilimo, usalama wa chakula, nishati, biashara na uwekezaji pamoja na mabadiliko ya tabianchi.

Ahadi hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa, Bjørg Sandkjær alipokutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Amesema, “katika hii ziara Naibu Waziri anatagemea kufanya ziara ya kutembelea hospitali ya Kiluteri ya Hydom ambayo imekuwa ikifadhiliwa na Serikali ya Norway madhumuni ya zaira hiyo ni kuangalia ni kwa namna gani Norway inaweza kuongeza ushirikiano na kuisaidia hospitali hiyo.”

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa Bjørg Sandkjær amesema kuwa ameitembela Tanzania kutokana na ushirikiano imara uliopo baina yake na Serikali ya Norway uliodumu kwa muda mrefu na ulianza kama ushirikiano wa maendeleo.

“Lengo la ziara yangu hapa Tanzania ni kuangalia ushirikiano katika sekta ya afya kwa sababu Norway imekuwa ikifadhili sekta, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, mifuko ya kimataifa, wadau wengine wanaohusika katika sekta ya afya pamoja na asasi za kiraia zinazofanya kazi na Serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za afya,” alisema Sandkjær.

Tanzania na Norway zimekuwa zikishirikiana katika sekta za afya, elimu, uvuvi, nishati jadidifu, kilimo, ushafirishaji na utalii pamoja na masuala ya bahari.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Machi 24, 2023
Sloti mpya ya Kasino ya Mtandaoni Inatoa Mpunga